Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa mikoani watinga Kubwa Kuliko

62805 KUBWA+PIC

Sat, 15 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

WANACHAMA wa Klabu ya Yanga wamejitokeza kwa wingi kwenye shughuli ya klabu hiyo ya Kubwa Kuliko inayofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya wanachama wengi kueleza kuwa wametoka mikoa mbalimbali nchini.

Lengo la shughuli hiyo ni kuchangia timu inayaokabiliwa na ukata ambapo klabu hiyo ilianza kuyumba kiuchumi tangu aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji kujiuzuru.

Wakati wakiwa wanaanza kutambulisha watu waliojitokeza ukumbini, ndipo wanachama hao walianza kutambulishwa kwa kunyanyuliwa kila meza.

Wanachama hao waliokuwa wanatambulishwa wametokea mikoa ya Mwanza na Dodoma ambao wamekuja kuunga mkono wanachama wenzao ili kufanikisha lengo lao.

Msimu uliopita timu ya Yanga ikiendeshwa kwa michango midogo midogo ndipo walipoamua kuandaa  tamasha ambalo lengo ni kupata pesa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

ujao.

Chanzo: mwananchi.co.tz