Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Singida United, Simba wasaka tiketi mageti yafungwa

Mashabiki wa Singida United, Simba wasaka tiketi mageti yafungwa

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mashabiki Singida United na Simba wamekwama kuingia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutokana na kuchelewa kuuzwa kwa tiketi pamoja na kufungwa kwa mageti ya uwanja huo.

Milango ya uwanja huo uliokuwa unatumika kwa shughuli za tamasha la muziki la Fiesta hadi mchana huu ilikuwa imefungwa kupisha shughuli za usafi wa uwanja.

Mbali na mageti kufungwa pia uuzaji wa tiketi hadi saa sita mchana hali ulikuwa wa kusuasua na kusababisha kero kwa mashabiki waliojazana getini kuhitaji tiketi hizo ikiwa ni saa manne tu kabla ya mchezo kuanza.

"Hapa wanataka kutengeneza hali ya fujo tu baadae watakapoanza kuuza tiketi muda wa mchezo ambapo itasababisha watu kusukumana na wengine kuzua vurugu watakapokata tiketi wakakose nafasi ya kukaa ndani" alisema Ramadhani Omary mmoja wa mashabiki wanaosubiri tiketi

Alisema tiketi yangefaa kuuzwa tangu jana au asubuhi watu walipokuwa wachache.

"Mimi nadhani huku ni kutokujipanga tu na kukosesha mashabiki katika mchezo huu, mfano sisi tumetoka Manyara alfajiri tumefika hapa saa tatu na uchovu wa safari halafu mtu akuweke getini baadae ukose tiketi kama si kuleta vurugu kwa hasira ni nini, niwaambie wazi kama wanataka kufanya mchezo wowote mbaya wakitegemea polisi wajue kabisa hawatasaidia baadae mbele ya hasira za watu wanaotoka mbali," alisema Richard Shija

Pia Soma

Advertisement
Meneja wa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Abdallah Kajembe alisema wamefunga uwanja ili kufanya usafi na makopo ya vinywaji vilivyotumika usiku wa kuamkia leo katika tamasha la fiesta pia kuondoa vitu hatari katika eneo la kuchezea kama vyuma na chupa na kusawazisha nyasi pia kuzibua vyoo vilivyotumika.

Katibu mkuu wa chama cha soka mkoa wa Arusha, Zakayo Mjema alisema kuwa uuzwaji wa tiketi utaanza muda siyo mrefu baada ya taratibu za awali kukamilika.

"Tulijipangia hivyo maana kuna mambo ya maandalizi hayajakamilika hivyo vuteni subira kidogo tiketi zitaanza kuuuzwa na mashabiki wataruhusiwa kuingia baadaa ya muda mfupi."

Chanzo: mwananchi.co.tz