Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki mechi ya Simba, Yanga kuvaa barakoa

1dbe0771d4d2a35794c53a1cdf59c3d5 Mashabiki mechi ya Simba, Yanga kuvaa barakoa

Sat, 3 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mashabiki watakaohudhuria mechi ya Ligi Kuu ya watani wa jadi Simba na Yanga Julai 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam wametakiwa kutakasa mikono yao kabla ya kuingia uwanjani na kuvaa barakoa kuepuka maambukizi ya corona.

Taarifa ya Bodi ya Ligi kuu Tanzania (TPLB) imesema mashabiki na wadau wote watatakiwa kuhakikisha wanatakasa mikono yao kabla ya kuingia uwanjani na kuvaa barakoa wakati wote wawapo uwanjani kujinga dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Bodi hiyo imewakumbusha mashabiki na wadau wote wa mpira wa miguu wanaohudhuria viwanjani kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania Bara kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata taratibu zote za kijilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya kcorona.

Katika hatua nyingine Bodi ya Ligi imesema mabasbiki wote walikata tiketi kwa ajili ya mchezo wa awali Simba na Yanga ulioahirishwa Mei 8 tiketi zao zimerejeshwa kwenye kadi zao (N-CARD).

Mashabiki hao watazitumia tiketi hizo kuingia uwanjani kwenye mchezo wa Julai 3 katika madaraja waliyolipia hapo awali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz