Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki elfu 10, kuishuhudia Simba na AS Vita

Shabiki Mashabiki elfu 10, kuishuhudia Simba na AS Vita

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Klabu ya Simba imethibitisha kuwa mashabiki Elfu kumi wataruhusiwa kuingia uwanjani kuushuhudia mchezo wao wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vitala ya Kongo, mchezo utakao chezwa Aprili 3, 2021, katika dimba la Mkapa Dar es salaam, mchezo huu utachezwa Saa 10:00.

Submitted by George David on Alhamisi , 1st Apr , 2021 Mashabiki wa Simba SC

Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbra Gonzalez amethibitisha kuruhusiwa kwa mashabiki kwenye mchezo huo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari walipokuwa wakizungumzia maandalizi kuelekea mchezo huo,

Leo tumepata habari njema kutoka CAF kuwa tumeruhusiwa mashabiki 10,000 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club. Hii ni fursa ya kipekee ambayo tumeipata, hakuna timu imeruhusiwa kwa idadi hii masharti ni mengi na lazima tuzingatie taratibu walizoweka ikiwemo kila shabiki kuingia akiwa amevaa barakoa."

Simba ilicheza bila mashabiki kwenye mchezo wake wa nyumbani uliopita dhidi ya Al Merrikh ya Sudan, ambapo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza msimu huu mabaingwa hawa wa Tanznaia kucheza bila mashabiki, kwa kile kilichotajwa kuwa ni kuzingatia kujikinga na maambukizi ya Covid-19, licha ya mashabiki kuruhusiwa lakini kuna masharti magumu sana yamewekwa hivyo wanapaswa kuyazingatia ili kuhakikisha michezo inayofata pia inakuwa na mashabiki.

Simba ndio vinara wa kundi A wakiwa na alama 10, Al Ahly ya Misri wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 7 AS Vital wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 4 na AL Merrikh ya Sudan ndio wanaburuza mkia wakiwa na alama 1.

Chanzo: eatv.tv