Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Simba, Yanga waungana kuimaliza Pyramids

81733 Pic+yanga Mashabiki Simba, Yanga waungana kuimaliza Pyramids

Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

IKIWA ni tofauti na siku za nyuma kwa mashabiki wa Yanga na Simba kuwa kitu kimoja hasa klabu mojawapo inapokuwa dimbani kucheza na timu nyingine, kuelekea mtanange wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mambo yamekuwa tofauti jijini hapa. Yanga wakiwa kama wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa hivi sasa, keshokutwa Jumapili watakuwa uwanja wa CCM Kirumba kumenyana na Waarabu wa Misri, Pyramids. Kuelekea katika mtanange huo mashabiki wa timu hizo kongwe nchini, wamezungumza na MCL  Digital kwa nyakati tofauti na kubainisha kuwa wataiunga mkono Yanga katika pambano hilo ambalo kwa upande wao wanaona kama ni bahati mechi hiyo kuchezewa jijini hapa. "Mimi ni shabiki wa Simba, lakini kwasababu mechi hiyo ni ya kuwakilisha Nchi, nitaenda uwanjani kuwapa sapoti Yanga, japokuwa safu yao ya ushambuliaji inasuasua lakini najua watatumia vyema Uwanja wa nyumbani kupata ushindi" amesema Paul Mseti. Kwa upande wa Mussa Misobi amewashukuru viongozi wa Yanga kuchagua uwanja huo kuchezea pambano hilo, aliongeza licha ya mshambuliaji wao Meib Kalengo kuumia na kukosa pambano hilo lakini bado anaamini watapata ushindi. " Waarabu utawashinda tu ule Uwanja, kwa mfumo wa kocha Mwinyi Zahera wa kupiga mipira mirefu utatusaidia, japokuwa mechi itakuwa ngumu lakini ushindi upo" amesema Misobi.

Chanzo: mwananchi.co.tz