Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mara inavyotisha Taifa Cup

Mara Inavyotisha Taifa Cup Mara inavyotisha Taifa Cup

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Timu ya kikapu ya wanawake ya Mkoa wa Mara inaendelea kutisha katika mashindano ya Kombe la Taifa baada ya kuifunga Arusha jana jioni kwa pointi 63-59 katika Uwanja wa Chinangali mjini Dodoma.

Ushindi wa timu hiyo ni wanne mfululizo kwani katika mchezo wa kwanza iliifunga Iringa kwa pointi 69-43, Dodoma 49-42, Mbeya 64-39 na Arusha 63-59.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa simu kutoka Dodoma, katibu mkuu wa kikapu mkoani humo, Koffison Pius alisema ushindi umetokana na juhudi za wachezaji kujituma katika michezo mitatu waliyocheza

Hata hivyo, alisema ushindani umekuwa mkubwa kwa timu zote zinazoshiriki mashindano hayo.

“Kwa kweli upande wetu tumejipanga vizuri kubeba kombe mwaka huu," alisema Pius.

Bosi huyo wa kikapu wa mkoa huo alisema kuna wadau wengi wamekuwa na kikapu bega kwa bega huku akimtaja mbunge wa Viti Maalumu, Esther Matiko kufanya nao kazi kubwa ikiwamo kuwatia moyo wachezaji wa timu hiyo ili kuhakikisha kwamba wanashinda michezo.

Mbunge huyo ana rekodi tamu katika mchezo huo kwani ni miongoni mwa mastaa wanaotisha katika ufungaji kwenye eneo la mitupo mitatu

“Unajua Esther ni mchezaji pia wa timu ya Mkoa wa Mara ambaye ni fundi wa ufungaji katika maeneo ya mitupo mitatu," alisema Pius.

Michezo mingine iliyochezwa upande wa wanawake ni kwa Unguja kuifunga Mbeya pointi 34, Dodoma imeifunga Iringa pointi 44-37 ilhali upande wa wanaume Iringa imeifunga Shinyanga kwa pointi 66-55.

Chanzo: Mwanaspoti