Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manura Awekewa Nusu Bilioni Mezani

Aishi Manula 13ka8rl8t6svv18tyvfrcys16m?fit=1200%2C800&ssl=1 Manura Awekewa Nusu Bilioni Mezani

Mon, 19 Apr 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

UONGOZI wa timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, umeweka mezani kitita cha Sh milioni 500, ili kuishawishi Bodi ya Wakurugenzi ya Simba chini ya mwenyekiti, Mohamed Dewji, wamuachie kipa, Aishi Manula.

Hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Mamelodi kuanza kumsaka mrithi wa kipa wao, Denis Onyango raia wa Uganda ambaye anaelekea kustaafu akiwa na miaka 35 hivi sasa.

Hivi karibuni, Onyango alitangaza kustaafu kucheza soka ngazi ya timu ya taifa, jambo lililowafanya Mamelodi kuanza mapema kujiandaa na maisha bila ya kipa huyo mkongwe aliyedumu hapo tangu mwaka 2011.

Ubora wa Manula, umezidi kuwavutia wababe wengi wa soka ndani ya Afrika wakitaka saini yake, baada ya msimu huu kufanya maajabu hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kiasi cha kuzidisha ofa ambapo mwanzo alikuwa akifukuziwa na Waarabu kutoka Sudan, Al Merrikh.

Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinasema kwamba, baada ya Al Merrikh kutangaza dau la zaidi ya Sh milioni 230 na mshahara wa Sh milioni 18 ili kumpata kipa huyo, sasa Wasauz nao wameingilia kati na kutangaza kutoa zaidi ya Sh milioni 500 ambayo ni nusu bilioni ili wamsajili kama mbadala wa Onyango.

Chanzo chetu kimelipenyezea Spoti Xtra kwamba: “Huwezi kuamini, Mamelodi wameonesha nia ya dhati ya kutaka saini ya Manula kwa kiasi cha shilingi milioni zisizopungua 500.

“Wanataka akawe mbadala sahihi wa kipa Mganda, Denis Onyango mwenye umri wa miaka 35 ambaye tayari ameshatangaza kustaafu kwenye timu yao ya taifa na huku akionesha nia ya kuachana nao pia.

”Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alizungumzia usajili wa Manula akisema: “Hatuwezi kumzuia mchezaji kuondoka, kinachotakiwa ni kufuata tu utaratibu kwa wanaomtaka, walete ofa, tuone kama inatufaa na mchezaji akikubali basi tunamruhusu.“Unajua sisi Simba hatuzuii mchezaji kuondoka, haya ni maisha yao, tupo tayari kumruhusu yeyote kuondoka lakini lazima taratibu zifuatwe.”

STORI NA MUSA MATEJA | GPL

Chanzo: globalpublishers.co.tz