Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula arudishwa Stars, sura mpya kibao

86458 Pic+stars Manula arudishwa Stars, sura mpya kibao

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars',  Ettiene Ndayiragije amewaita wachezaji 32 kuunda kikosi kitakachoshiriki mashindano ya Chalenji yatakayofanyika Uganda. Mashindano hayo ya Cecafa yataanza kutimua vumbi Disemba 7 mwaka huu huku kipa wa Simba, Aishi Manula akijumuishwa kikosini hivyo timu hiyo kuwa na makipa wanne wakiongozw ana Juma Kaseja wa KMC, Metacha Mnata (Yanga) na David Kisu (Gor Mahia ya Kenya). Wachezaji wengine ni Salumu Kimenya, Mkandala Cleoface wote kutokea Tanzania Prison, Juma Abdul, Kelvin Yondan (Yanga), Gadiel Michael, Jonas Mkude, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na Miraji Athumani kutoka Simba. Wengine ni Mwaita Gereza, Zawadi Mauya, Yusuph Mhilu (Kagera Sugar), Fred Tangalu, Paul Nonga (Lipuli), Idd Seleman, Salum Abubakar, Shaban Chilunda(Azam), Baraka Majogoro na Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania). Wengine Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union, Abdulmajid Mangalo (Biashara United),  Jafar Kibaya (Mtibwa Sugar) na Kikoti Lucas (Namungo). Wachezaji watatu wanaocheza nje ya Tanzania walioitwa ni Nickson Kibabage wa Difaa El Jadid ya Morocco, Kelvin John kutokea Football House, Eliud Ambokile (TP Mazembe ya DR Congo) na Eliuter Mpepo (Buildcom Zambia). Katika kikosi hiko Manula, amerejea baada ya kukosekana katika timu ya Taifa Stars, iliyocheza mechi ya kufuzu Chan na Afcon, wakati huo huo kuna sura mpya kama Abdul, Kikoti, Gereza, Ambokile, Kibabage, Mkandala, Mhilu, Nonga, Kibaya na Tangalu.

Chanzo: mwananchi.co.tz