Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula anakosea hapa, Kaseja na Metacha wao wanapita hapa

80965 Manula+pic Manula anakosea hapa, Kaseja na Metacha wao wanapita hapa

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Juma Kaseja anayechezea KMC na Metacha Mnata ni miongoni mwa makipa wawili ambao wamo kwenye kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ambacho jana kilikuwa na mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan).

Mbali na Kaseja na Metacha, makipa wengine wawili wanaounda kikosi cha Taifa Stars ni vijana Said Kipao anayedakia Kagera Sugar na Razack Shekimweli wa kikosi cha vijana cha Mtibwa Sugar, ambaye pia anadakia timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ‘Ngongoro Heroes’ iliyotwaa ubingwa wa mashindano ya Cecafa.

Baadhi ya watu wanashangaa kutoitwa kikosini kwa kipa wa Simba, Aishi Manula ambaye anahesabika kama miongoni mwa makipa wa daraja la juu kwa kizazi cha sasa hapa nchini.

Ni jambo lisilo na kificho kwamba Manula ni kipa mzuri na ambaye amekuwa akionyesha kiwango bora katika mechi mbalimbali za ngazi ya klabu au hata pale alipokuwa anaidaikia Taifa Stars na pia vikosi vya timu za taifa za vijana.

Hata hivyo, kasoro ambayo pengine inamkwamisha Manula hadi tunaona benchi la ufundi la Stars halimjumuishi kwa sasa ni kutozungumza pindi awapo uwanjani, sifa ambayo naamini wenzake akina Kaseja na Metacha Mnata wanayo.

Tunasema kipa ni ‘Commander-in-Chief’ au kiongozi wa timu ndani ya uwanja kwani yeye ndiye anaiona timu kiujumla, hivyo ndiye ana nafasi kubwa ya kuwakumbusha wenzake majukumu yao pindi anapoona wamekosea.

Pia Soma

Advertisement
Uwezo huo wa kuisoma timu pinzani tunaita ‘Game Reading and Understanding’ (kuusoma mchezo na kuuelewa).

Kuna sifa au majukumu 11 ambayo mchezaji anayecheza nafasi ya kipa anapaswa kuwa nazo ambazo zimegawanyika katika majukumu makubwa manne, ambayo benchi la ufundi huyatumia kufanya uamuzi wa nani anaaze au nani asianze kwenye nafasi hiyo.

Jukumu la kwanza kati ya hizo nne ni kuzuia mpira kuingia kwenye nyavu zake na hili analifanya kwa kutumia kiungo chochote kile na la pili tunasema clearing of the ball (kuondosha mpira) pale ambapo lango lake linakuwa linashambuliwa.

Lakini pia jukumu lingine ni directing his/her teammates (kutoa maelekezo kwa wachezaji wenzake) na jambo au jukumu la nne ni balls distributions (usambazaji wa mipira).

Kipa anatakiwa awe na uwezo wa hali ya juu wa kusambaza mipira na kuianzisha pale anapokuwa nao.

Kiufundi kipa anaingia kwenye idara ya ulinzi ambayo ni mojawapo ya idara tatu za msingi ndani ya uwanja, nyingine zikiwa ni ya kiungo na ushambuliaji.

Ufanyaji kazi wa idara hizi ndani ya uwanja unatengeneza kitu kinaitwa ‘transitional movement’ ambacho ni namna ambavyo timu inaweza kutimiza majukumu mawili ndani ya uwanja - ambayo ni jukumu la kujilinda pale wapinzani wanapokuwa na mpira na lile la kushambulia wakati ambao inakuwa na mpira.

Kipa ni eneo linalohitaji kitu kinachoitwa courage (ujasiri) kwa sababu kuna nyakati atalazimika kukabiliana na washambuliaji wa timu pinzani ana kwa ana.

Lakini pia kipa anatakiwa awe na timing (hesabu) nzuri pindi anapokuwa langoni. ‘Timing’ ndio inamwezesha kujua ni wakati gani wa kutoka langoni au wakati gani hapaswi kutoka, azuie shambulizi kwa mikono au kiungo kingine na alipunguze vipi lango ili kumnyima fursa mshambuliaji wa timu pinzani.

Yote kwa yote, kipa anatakiwa awe na passion (utayari) ya kucheza kwenye nafasi hiyo kwa sababu ndio utamfanya ajitume na kujitolea mazoezini na kwenye mechi.

Kiujumla Tanzania kwa sasa tuna kundi kubwa la makipa wazuri na nadhani hili linachochewa na mambo kadhaa. Moja ni upekee wa nafasi yenyewe kwa maana kwamba, ni rahisi kwa kipa kuonekana pindi akifanya vizuri kwa sababu nafasi hiyo anacheza peke yake, lakini pia naamini wanatimiza maadili ya kazi yao wakiamini itawasaidia kucheza kwa muda mrefu.

Ikumbukwe kwamba kadri wanavyocheza na umri wao kusogea, wanaongezeka ujasiri ambao unawafanya wazidi kuwa makipa wazuri. Mtazame Buffon, Petr Cech na Edwin van der sar ambavyo wametamba wakiwa na umri mkubwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz