Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula,Bocco na Said Ndemla wala tuzo mbele ya Ubalozi wa Uturuki

2522 26871785 363833757422003 287296237944700928 N

Sat, 3 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya soka ya Simba hapo jana imewapatia tuzo wachezaji wake ambao wamefanya vizuri kufuatia michezo mbali mbali waliyo cheza.



Katika ghafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovutoglu pamoja na Mkewe Bi. Ye?im Meço Davutoglu walimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mlinda lango namba moja ndani klabu ya Simba, Aishi Manula.

Lakini pia balozi, Ali Dovutoglu aliwakabidhi medali wachezaji bora wa mechi nne zilizopita nahodha John Bocco na Kiungo Said Ndemla ambao walishinda kufuatia kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Singida United, Kagera Sugar, Ndanda FC na Majimaji FC.



Tuzo hizi zimetolewa katika hafla maalumu iliyoandaliwa na Ubalozi wa Uturuki kwa ajili ya kujenga na kuimarisha ushirikiano mzuri kati ya klabu ya Simba na nchi hiyo.

Chanzo: bongo5.com