Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula Akubali 230M za Waarabu

Video Archive
Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Manula Akubali 230M za Waarabu April 2, 2021 by Global Publishers



PAMOJA na Kocha Mkuu wa Simba, raia wa Ufaransa, Didier Gomes Da Rosa, kusema hayupo tayari kumuachia kipa wake, Aishi Manula, ajiunge na Al Merreikh ya Sudan, mwenyewe amesema akiruhusiwa na viongozi hata leo anaondoka.

Ni zaidi ya wiki tatu sasa, Waarabu hao wa Sudan kupitia rais wao, Adam Sudacal, wamekuwa wakionesha nia ya kuhitaji saini ya Manula na kutangaza dau la zaidi ya shilingi milioni 230, na mshahara shilingi 18M.

Dili la Manula kwenda Al Merrikh, limependekezwa na kocha wa timu hiyo, Lee Clark, baada ya kuvutiwa na kiwango chake kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Manula ameliambia Spoti Xtra kuwa, kwa sasa yuko tayari kuitumikia timu yoyote inayomuhitaji, kikubwa wanaomtaka wamalizane na uongozi wake, kwani bado ana mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja.

“Ni kweli kuna ofa nyingi nimesikia na mimi kama mchezaji najisikia furaha kusikia kuna timu zimevutiwa na huduma yangu, ila tatizo ni kwamba siwezi kwenda popote bila ruhusa ya viongozi wangu wa Simba, kwani mimi si mchezaji huru, bado nina mkataba,” alisema Manula.

STORI NA MUSA MATEJA | GPL

Chanzo: globalpublishers.co.tz