Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba atakosa michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia, baada ya kupata jereha la paja na hivyo atakosa michezo dhidi ya Kazakhstan siku ya Jumamosi pamoja Finland siku ya 16 November.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia, 28, alipata jeraha hilo akiwa mazoezini siku ya Jumatatu, Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) lilisema.
Mchezaji huyo wa zamani wa Juventus, alikuwa tayari nje ya mipango ya mechi inayofuata ya United, ugenini dhidi ya Watford kwenye EPL mnamo Novemba 20, huku akikamilisha adhabu yake ya kadi nyekundu kwenye mechi tatu.
Pogba alitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati Liverpool ilipowaadhibu mabao 5-0 na Oktoba 24.
FFF ilisema Pogba alikuwa "anasumbuliwa na jeraha kwenye paja la mguu wa kulia".
Ufaransa inahitaji ushindi mmoja kutoka katika michezo yao miwili iliyosalia ili kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022.
Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer tayari hana wachezaji kadhaa kwa sababu ya majeraha.
Mchezaji mwenzake wa kimataifa, Raphael Varane yuko nje kwa sababu ya jeraha la misuli ya paja, fowadi Edinson Cavani alikosa kichapo kutoka kwa Manchester City Jumamosi iliyopita, huku Luke Shaw akitolewa katika mechi hiyo.