Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manchester United yapata janga, Mourinho akubali kushushwa na Chelsea

866 DSUm I7X0AIjRJr TZW

Mon, 1 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya Manchester United bado imeendelea kupata matokeo mabovu kwenye Ligi Kuu soka England baada ya jana kulazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya klabu ya Southampton.

Jose Mourinho

Kwa matokeo hayo Manchester United ambayo ilikuwa nafasi ya pili kwa muda mrefu kwenye msimamo wa EPL imeshuka hadi nafasi ya tatu baada ya Chelsea jana kupata ushindi mnono.

Wakati hayo yakitokea Manchester United imepata janga lingine kubwa zaidi kwa kuumia mchezaji wao tegemezi, Paul Pogba jana kwenye mchezo huo.

Pia kupitia mtandao wa klabu hiyo umethibitisha kuwa mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovi? kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kuanzia jana.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kupata sare tatu mfululizo kwenye EPL na kupoteza mechi moja ya kombe la EFL.

Matokeo mengine ya ya mechi za jana za EPL ni kama ifuatavyo.

 

Chanzo: bongo5.com