Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara azimia mara mbili baada ya kichapo cha Kaizer Chiefs

Manara Pic Data Manara azimia mara mbili baada ya kichapo cha Kaizer Chiefs

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

PRETORIA, AFRIKA KUSINI. ILIKUWA siku ngumu kwa Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara baada ya kuzimia mara mbili katika hoteli ya Sky ambayo Simba ilikuwa imefikia jijini Johannesburg kufuatia kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Kaizer Chiefs.

Manara alianza kujisikia vibaya mara baada ya kuwasili hotelini akitokea katika

Uwanja wa FNB ambako pambano hilo lilifanyika. Madaktari wa Simba walilazimika

kumpa huduma ya kwanza kwa saa zima msemaji huyo ambaye ni mtoto wa staa wa zamani wa Yanga, Sunday Manara

“Nimezimia mara mbili. Hali yangu ilikuwa mbaya nusura nife. Nina presha ya kushuka na mara nyingi huwa natumia chumvi kujiweka sawa. Hali yangu kwa sasa ni nzuri lakini huu mpira unaweza kutuua siku moja,” alisema Manara.

Simba ilikubali kichapo hicho na kujiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika huku pambano la marudiano likitazamiwa kufanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz