Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara awataka mashabiki Simba kujaza Uwanja Taifa

32205 Pic+manara Mashabiki wa Simba

Tue, 18 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mashabiki wa Simba wameombwa kuujaza uwanja Jumapili katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kati ya Simba na Nkana Red Devil's ya Zambia utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Wapinzani wa Simba, Nkana wanatarajiwa kuwasili leo Jumanne usiku kwa ndege ya Shirika la ndege la Kenya.

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amewaangukia mashabiki kwenda kuisapoti timu hiyo kwa kuujaza Uwanja wa Taifa kama ilivyokuwa katika tamasha la Simba Day lililofanyika Agosti 8.

"Tulivyokuwa Zambia licha ya Uwanja wa Nkana kuwa mdogo, lakini mashabiki wao walikuja kwa wingi na kushangilia muda wote wa mchezo. Hata tulipopata bao sisi waliendelea kushangilia.

"Sasa niwaombe mashabiki wetu na wapenda soka, waje kwa wingi Jumapili waujaze uwanja ule, sapoti yao inahitajika sana kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe.

"Hiyo ni mechi ya kufa au kupona kwani tukishinda tunafuzu makundi hivyo lazima tushirikiane kuanzia viongozi, mashabiki na wachezaji.

"Waje kwa wingi, uwanja ujae, washangilie muda wote, tuwape nguvu wachezaji ili nao waifanye kazi yao vizuri na kutupatia ushindi"alisema Manara.

Manara alisema Alhamis atakutana na viongozi wote wa vikundi vya ushangiliaji vya Simba ili kujipanga kwa ajili ya Jumapili.



Chanzo: mwananchi.co.tz