Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara asisitiza hakuna timu isiyofungwa

MANARA Manara asisitiza hakuna timu isiyofungwa

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Uongozi wa Klabu ya Yanga umewataka mashabiki na wanachama wake kutorudi nyuma katika kuiunga mkono timu yao hata kama haitopata matokeo ya kuwafurahisha katika msimu huu wa mashindano ulioanza mapema wiki hii.

Submitted by George David on Jumamosi , 2nd Oct , 2021 Msemaji wa Yanga, Haji Manara.

Kupitia Msemaji wa Yanga, Haji Manara, amesekuwa hakuna timu ambayo haifungwi, au kutoka sare lakini kwakuwa Ligi ina michezo mingi anaamini kikosi chao kipo imara kwa ajili ya kutwaa mataji likiwemo la Ligi Kuu Tanzania bara.

Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya Yanga kuanza vyema Ligi ikishinda kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Manara amesema kumekuwa na kasumba ya mashabiki kulalamikia ushindi mdogo, au timu ikifungwa wanapunguza kujitokeza uwanjani kuwapa hamasa wachezaji wao, jambo ambalo halina faida kwa timu.

Chanzo: eatv.tv