Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara aonya Ligi Kuu ikirejea

23220 Manara+pic Manara aonya Ligi Kuu ikirejea

Tue, 19 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Hajji Manara, amewataka wadau wa soka kuchukua tahadhari na kuzingatia maelekezo ya kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona, pindi Ligi Kuu Bara itakaporejea.

Manara ametoa kauli hiyo, baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk. John Magufuli, juzi kusema kama hali ya maambukizo ya virusi vya corona itaendelea kuwa ya chini kama ilivyo sasa, ataruhusu ligi nchini kurejea hata wiki hii.

"Kauli ya mheshimiwa rais kurejesha ligi haina maana tusichukue tahadhari juu ya janga hili, hivyo tutakaporejea tunatakiwa kuzingatia maelekezo ya mamlaka husika juu ya kuchukua tahadhari ya kujilinda na ugonjwa huu," alisema Manara.

Alisema wamepata faraja kubwa na kauli hiyo wakiwa kama wadau wa soka na wameipokea kwa furaha kubwa, lakini rais amelisaidia Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutua mzigo mkubwa juu ya nani ataiwakilisha nchini katika michuano ya kimataifa endapo ligi ingefutwa.

"Nadhani hili TFF hawajaliweka wazi, ila kwa utamaduni wetu Tanzania ingekuwa maneno kuwa Simba imebebwa endapo ingepewa nafasi hiyo kama ilivyo kwa mataifa mengine kuwapa nafasi timu inayoongoza ligi au bingwa mtetezi," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live