Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara anyoosha mikono kwa Senzo

Simba 8 Manara anyoosha mikono kwa Senzo

Wed, 13 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara, ameshindwa kuzuia hisia zake na kumtaja bosi wake, Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O), kuwa ni kati ya viongozi wachapa kazi.

Senzo raia wa Afrika Kusini, aliyetua nchini mwaka jana, amekuwa nyuma ya mafanikio ya Simba msimu huu ambayo inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 71.

Katika ukurasa wake wa instagram wakati wa kumtakia heri ya kuzaliwa, Manara, aliandika kuwa, kwa miezo saba aliyokaa na Senzo, amejifunza mambo mengi kutokana na kiongozi huyo kulifahamu vizuri soka la Afrika.

Manara alisema amegundua kuwa CEO huyo, yupo makini katika kufanya kazi yake inavyotakiwa pia ana ushirikiano mkubwa na watu wanaomzunguka ndani na nje ya kazi.

“Kwa miezi saba niliyofanya kazi na huyu mtu (Senzo), nimegundua na kujifunza vitu vingi sana, jamaa anajua soka na utawaka wake, ana ushikiano katika kazi na nje ya kazi.

“Ni mtu muungwana na hodari kusoma mazingira, hakika Simba imepata mtu sahihi kwa nafasi ya C.E.O wa klabu,” alisema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live