Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara alianzisha Lesotho

27735 Pic+manara TanzaniaWeb

Tue, 20 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Msafara wa mashabiki wa Tanzania unaondoka muda huu kuelekea uwanjani tayari kwa kuishangilia Taifa Stars inayocheza na Lesotho saa 11 jioni.

Mashabiki hao wanaanza msafara huo katika Hoteli ya Avoni hadi kwenye Uwanja wa Taifa wa Lesotho uliopo katikati ya jiji la Maseru.

Kabla ya kuanza kwa msafara huo,Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliyeingia jijini Maseru jana usiku, aligeuka kivutio kutokana na jinsi alivyokuwa anawajaza molali na hamasa mashabiki.

Manara aliyezungukwa na kundi kubwa la watu, alisema kuwa wamefunga safari kutoka Dar es Salaam kuja Lesotho kwa kazi moja tu ya kuwamaliza wenyeji.

Zaidi ya magari nane yaliyowajaza Watanzania yameunga msururu mrefu kuelekea uwanjani



Chanzo: mwananchi.co.tz