Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo ya kukumbukwa Kombe la Dunia Afrika

8919 KOMBEEEE TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moscow, Russia. Kombe la Dunia lililofanyika Afrika ya Kusini mwaka 2010 lina mambo mengi ambayo yameweka alama na yanakukumbukwa kila zinapofika fainali kama hizo.

Timu ya Taifa ya Hispania ndiyo iliyotwaa taji lake la kwanza la ubingwa huo wa dunia, huku Andres Iniesta akifunga bao lake dakika ya 16 alipoifungia timu yake dhidi ya Uholanzi na lilidumu hadi mpira unamalizika.

Pia, itakumbukwa katika mashindano hayo Ujerumani ilitwaa medali ya shaba baada ya kumaliza nafasi ya tatu huku raia wa Uruguary, Diego Forlan aliibuka kinara wa ufungaji mabao akizawadiwa mpira wa dhahabu wa Adida.

Mchezaji bora chipukizi nafasi ilikwenda kwa Mjerumani Thomas Muler.

Hispania ilitwaa taji hilo ikiwa imetenganishwa takriban kilometa 12 tu na linapoanzia bara la Afrika kwenye ramani. Licha ya wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini  kulikosa kombe hilo lakini walishangilia kwa nguvu ushindi wa Hispania katika fainali hizo zilizofanyika kwa mara ya  19.

Jambo jingine ambalo halitasahaulika kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika bara la Afrika, ni ukarimu na ucheshi wa wenyeji kwa wageni hasa kuwapa sapoti ya kushangilia mabingwa Hispania.

Hispania waliendeleza shangwe za ushindi wao kwenye dimba la Soccer City ambako ulikuwa ni uwanja zilipofanyika fainali hizo nchini Afrika Kusini.

Waafrika Kusini kwa upande wao walifanikiwa kuliweka vuvuzela kwenye ramani ya soka. Hivyo kila linapoonekana limekuwa likionyesha alama ya soka popote ulimwenguni kwa mashabiki wa mpira wa miguu.

Chanzo: mwananchi.co.tz