Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo matano yaliyochomoza Ligi ya Mabingwa Ulaya 2019

77026 Uefa+pic

Tue, 24 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kurejea kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 65, umekuwa na msisimko wa aina yake kutokana na matokeo yaliyopatikana katika michezo ya mzunguko wa kwanza.

Mabingwa wa kihistoria Real Madrid imeanza vibaya ligi hiyo kwa kupokea kipigo cha mabao 3-0 huku mabingwa watetezi, Liverpool wakikiona cha moto baada ya kufungwa na Napoli ya Italia mabao 2-0.

Kwa mara ya kwanza msimu huu wa 2019/2020, matumizi ya teknolojia ya VAR, imeanza kutumika na iliamua Chelsea kupewa penalti ambayo ilikoswa na mchezaji wa kiungo Ross Barkley katika mchezo waliofungwa bao 1-0 dhidi ya Valencia.

Pia VAR ilitumika kukataa bao la Real Madrid katika mchezo dhidi ya Paris Saint Germain (PSG), lililofungwa na Gareth Bale ambaye alishika mpira.

Wakati mashindano hayo yakianza kwa kutoa matokeo yasiyotarajiwa, mambo matano yamechomoza katika mechi za kwanza.

Bao la Kwanza

Pia Soma

Advertisement
Usiku wa Jumanne, Mnigeria Peter Olayinka alifunga bao la kwanza msimu huu wa Ligi ya Mabingwa nchini Italia ambapo SK Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech iliibana Inter Milan na kutoka sare ya bao 1-1.

Olayinka ambaye bao lake liliiweka mbele SK Slavia Prague dakika ya 63 ya mchezo huo kabla ya kusawazishwa na Nicolo Barella, pia aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Nigeria, kufunga katika ligi hiyo tangu Yakubu Aiyegbeni akiichezea Maccabi Haifa afunge matatu dhidi ya Olympiakos , Septemba 2002.

Hat- Trick ya Kwanza

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akiwa na KRC Genk alionja shubiri dhidi ya FC Red Bull Salzburg nchini Austria. Mabao matatu yalifungwa na kinda Erling Braut. Genk ilicharazwa mabao 6-2.

Erling, (19), alifunga mabao matatu ambayo yamemfanya kuingia katika rekodi ya kuwa mchezaji chipukizi wa tatu kufunga mabao matatu ‘hat trick’ katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kipigo Real Madrid

Real Madrid ambayo imetumia zaidi ya Euro 300milioni katika dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, imeshangaza namna ilivyopoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain.

Ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Parc des Princes, Ufaransa matajiri hao wa Hispania, walikumbana na kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya PSG, ambayo haikuwa na mastaa watatu Neymar, Kylian Mbappe na Edinson Cavani ambao ni majeruhi.

Real Madrid haitamsahau nyota wake wa zamani Angel Di Maria wa ambaye alifunga mabao mawili na jingine likifungwa na beki Thomas Meunier.

Rekodi ya Samatta

Samatta ameweka rekodi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Nyota huyo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza mashindano hayo makubwa ngazi ya klabu Ulaya.

Pia aliweka rekodi nyingine dakika ya 52 kufunga bao baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Theo Bongonda. Samatta anakuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kufunga bao katika ligi hiyo.

Bao hilo lilimfanya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kufunga bao lake la kwanza katika mchezo wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa.

Rekodi nyingine ni kuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kuadhibiwa katika mashindano hayo baada ya kulimwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Zlatko Junuzovi?.

Lewandowski

Mshambuliaji nguli Robert Lewandowski amefikisha mabao 200 akiwa na miamba ya soka Ujeruman, Bayern Munich.

Nguli huyo ameweka rekodi yake katika michezo 249. Alikuwa sehemu ya ushindi wa timu hiyo ambayo ilipata mabao 3-0 dhidi ya FK Crvena Zvezda huku.

Lewandowski alifunga bao katika mchezo huo ambao Bayern Munich ilicheza kwa kiwango bora licha ya kupata upinzani.

Raundi ya pili katika michezo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, itaendelea Oktoba mosi kwa mechi mbalimbali kupigwa na zinatarajiwa kuwekwa ikiwemo ya mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao katika ligi hiyo.

Mchezaji chipukizi anayewania rekodi hiyo ni Ansu Fati wa Barcelona. Winga huyo mwenye miaka 16, amefunga mabao mawili katika mechi mbili alizocheza Barcelona msimu huu.

Barcelona ilimsajili Ansu mwenye futi tano mwaka 2012 akitokea Sevilla ambapo alijiunga na klabu hiyo akiwa mtoto kabla ya mwaka huu kuanza kumtumia rasmi katika mechi zake

Chanzo: mwananchi.co.tz