Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama Samia anunue jezi Stars kwa Sh5 milioni

63561 Mamasamihapic

Thu, 20 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, amenunua jezi ya timu ya taifa 'Taifa Stars' kwa bei ya Sh 5 milioni.

Kiasi hicho cha fedha ni zaidi ya mara 16 ya gharama halisi ya jezi hiyo ambayo inauzwa kuanzia Sh30,000.

Mama Samia amenunua jezi hiyo ni mchango wake katika harambee ya kuichangia timu ya taifa 'Taifa Stars' inayoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) huko Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19.

Makamu wa Rais alisema kuichangia timu ya taifa ni jambo la fahari na hivyo yeye kama kiongozi ni lazima aonyeshe mfano kwa vitendo.

"Tulianzisha kampeni ya kuichangia timu ya taifa ya wanawake lakini kwa bahati mbaya mechi ya kwanza tu ikapoteza.

“Leo nimekuja hapa na Mjukuu wangu Mai ambaye amevaa jezi za timu ya taifa na amesema atachanga kiasi cha Sh 5,000 ila ameniambia anataka nami nimnunulie jezi ya timu ya taifa.”

Pia Soma

“Sasa kutokana na hilo, mimi nitanunua jezi ya timu ya taifa kwa Sh5 milioni na jezi ya mjukuu wangu Mai nayo nitainunua kwa kiasi cha Sh100,000," alisema Mama Samia.

Mara baada ya Makamu wa Rais kununua jezi hiyo kwa Sh 5 milioni, kampuni mbalimbali zimeendelea kumuunga mkono kwa kutangaza kiasi cha fedha zinachopanga kutoa kwa ajili ya jezi hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz