Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda aikabidhi Yanga nyaraka za Uwanja Kigamboni

63096 Pic+yanga

Tue, 18 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameihakikishia Yanga kumiliki Uwanja eneo la Kigamboni baada ya leo hii kuwakabidhi nyaraka za uthibitisho kuonyesha wao ni wamiliki halali wa uwanja huo.

Hafla ya kuwakabidhi cheti hicho cha utambuzi, imefanyika leo kwenye Hoteli ya Serena jijini ambako Makonda alikabidhi kwa mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi cheti hicho, Makonda alisema makabidhiano hayo yanatoa ishara njema kuwa serikali ina nia ya dhati ya kukuza michezo.

"Jumamosi iliyopita niliahidi kuipatia Yanga, uwanja eneo la Kigamboni na leo tumeanza mchakato wa kuwamilikisha Yanga eneo na siku ya Ijumaa rasmi eneo ili waanze ujenzi," alisema Makonda.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaya amemshukuru mkuu wa mkoa na serikali kiujumla kwa kuwapatia uwanja huo.

"Kwa upande wetu sisi Yanga tunamshukuru Mkuu wa Mkoa kwani jambo alilolifanya ni kubwa kwa faida ya klabu yetu na taifa kwa ujumla.

Pia Soma

“Tunangoja makabidhiano rasmi na baada ya hapo ndipo tutajipanga kuanza ujenzi wa uwanja," alisema Kaya

Chanzo: mwananchi.co.tz