Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda: Watu walinibeza niliposema nawapa Yanga eneo

63795 Pic+makonda+2

Sat, 22 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema alibezwa na baadhi ya watu alipotangaza kuipa Yanga eneo.

"Wapo waliosema nawapa eneo la Manji (Yusuf aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga ambaye alitangaza kuwapa eneo Gezaulole).

"Kuna watu kila mmoja aliongea lake, ilikuwa ni changamoto kubwa, lakini sasa nimekata mzizi wa fitina," alisema Makonda.

Alisema ametoa eneo hilo la ekari saba sanjari na lile la ekari 15 kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na mahaba aliyonayo katika soka nchini.

"Mimi ni shabiki wa Simba kindakindaki, lakini napenda maendeleo ya soka ndiyo sababu nimetoa maeneo hayo kwa Yanga na TFF," alisema.

Alisema anatamani kuona sasa TFF na Yanga wanayaendeleza maeneo hayo ikiwezekana kujengwe kituo cha mfano ambacho kitazivutia timu za nje ya nchi kuweka kambi hapo.

Chanzo: mwananchi.co.tz