Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makomandoo Yanga nusura wawachape maofisa TFF

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIDOGO zichapwe kati ya makomandoo wa Yanga na watu wa TFF   pindi ambapo kikosi cha timu hiyo kilipokuwa kinawasili Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Basi la Yanga liliwasili saa 10 kasoro na ghafla makomandoo wa timu hiyo wakashuka na kuanza kuwatawanya watu wa TFF  kwenye lango kuu la kuingilia.

Watu hao wa TFF,  walianza kuzozana na makomandoo wa Yanga waliokuwa na mzuka huku wakiwa wamevalia jezi za timu hiyo zenye rangi ya njano zikiwa na maandaishi yanayosomeka Yanga Observer.

Muda mchache akatokea Afisa mmoja wa Polisi ambaye aliwatuliza watu hao wa TFF  na makomandoo wa Yanga kibabe wakaliteka eneo hilo kisha wachezaji wao wakaanza kushuka kwenye basi na kuingia vyumbani.

Aliyeanza kushuka kwenye basi la Yanga alikuwa ni winga wa zamani wa Singida United, Deus Kaseke huku wa mwisho akiwa Ibrahimu Ajibu.

Chanzo: mwananchi.co.tz