Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makocha Biashara, Mwadui presha tupu

59916 Pic+presha

Tue, 28 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Simba ikisubiri kukabidhiwa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kesho, makocha wanane wanahaha kuzinusuru timu zao na janga la kushuka daraja.

Timu hizo ni JKT Tanzania (44), Biashara United (44), Stand United (44), Mbao (44) Prisons (43) Kagera Sugar (43), Ruvu Shooting (42) na Mwadui (41) ambazo ziko katika mazingira magumu ya kubaki Ligi Kuu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, Kocha wa Biashara United, Amri Said ambaye timu yake itacheza na Mbeya City, alisema amewaandaa kisaikolojia wachezaji wake kupata ushindi.

Alisema baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Simba jijini Dar es Salaam juzi, mkakati wake ni kupata ushindi katika mchezo huo.

Kocha wa Mwadui, Ally Bizimungu alisema mchezo wa ugenini dhidi ya Ndanda utaamua mustakabali wao kama watabaki au watashuka daraja

“Kikubwa ni kushinda wakati huo tukisubiri matokeo ya washindani wetu, ligi ilikuwa ngumu lakini lazima tupambane ili tusishuke,”alisema Bizimungu.

Pia Soma

Kocha Msaidizi wa Mbao, Fulgence Novatus alisema mechi ya mwisho dhidi ya Kagera Sugar itakuwa na ushindani mkali, lakini watapambana kupata pointi tatu.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime alisema ana matumaini ya kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ili kujinasua na janga la kuteremka daraja.

Timu ya African Lyon imekuwa ya kwanza kuteremka daraja baada ya kucheza chini ya kiwango cha chini.

Chanzo: mwananchi.co.tz