Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makipa Simba hawapoi! Nduda arudi mzigoni

15830 PIC+MAKIPA TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI cha Simba kwa sasa kuna makipa wanne ambao ni Aishi Manula, Deogratious Munishi, Ally Salim na Said Mohammed ‘Nduda’ ambaye hakuwa na kikosi hiko mwanzo wa maandalizi ya msimu mpya.

Nduda aliondoka katika kikosi cha Simba wakati wanacheza mashindano ya Kagame Cup ambayo Simba walifungwa katika mechi ya fainali na Azam mabao 2-1 na kukosa ubingwa huo.

Katika orodha ya wachezaji wa Simba waliowachwa msimu huu jina la Nduda halikuwepo na alikuwa miongoni mwa nyota ambao usajili wao unatambulika kuwa wapo katika kikosi hiko.

Nduda ambaye aliibuka mazoezini siku ya Jumanne ambapo Simba walifanya katika viwanja vya Gym Khana asubuhi na jioni na kukili kuwa changamoto ilikuwa mbele yake imemalizika.

Anasema kila binadamu anamapungufu yake ambayo yanaweza kumfanya kuchukua maamuzi yoyote yale hilo ndio ambalo lilimkuta hata yeye lakini limeshamalizika.

“Nimekaa na viongozi wangu kuwaeleza kila ambalo lilikuwa limenifanya kuamua maamuzi hayo ambayo yalinifanya kutokuwa na timu lakini nashuku wamenielewa na kunisamehe na kuniambia nirudi kazini,” alisema.

“Matatizo tu ambayo yamekwisha na nimekuja kazini kivingine kwani nataka kuhakikisha napata namba ya kucheza ingawa si jambo rahisi kwani ambao nashindana nao anauwezo pia,” alisema.

“Natambua uwezo wa Manula, Dida, Salim lakini kama mchezaji sitakiwi kukata tamaa natakiwa kutumia ubora wao kama changamoto kwangu ili kupata nafasi hiyo ya kucheza.

“Naimani niliondoka hapa kuna kocha mwingine lakini sasa yupo mpya na kama nitaonesha uwezo nafasi ya kucheza kwangu naiona ipo wazi,” alisema Nduda.

Kocha wa Simba Patrick Aussems alisema kwake kuwa na makipa wane haina shida kutoka mashindano ni mengi msimu huu lakini ambaye atakuwa bora kuliko wenzie ndio atapewa nafasi ya kucheza.

“Kama ilivyokuwa katika upana wa wachezaji wa ndani ndio hivyo kwa makipa nataka ambaye anafanya vizuri kwa kuonesha uwezo atacheza na si kuangalia jambo linguine,” alisema.

“Nimefurahi kumuona Nduda naimani amekuja kuongeza nguvu katika kikosi chetu na nimeongea nae asahau yote yaliyopita ila anatakiwa kuanza upya kwa kufanya kazi,” alisema Aussems.

Chanzo: mwananchi.co.tz