Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makahama yampoa Eto'o mtoto Ulaya

Erika Do Rosario Makahama yampoa Eto'o mtoto Ulaya

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama moja huko katika jiji la Madrid imemtaja gwiji wa soka wa Caméroon Samuel Eto'o kuwa baba mzazi wa mtoto wa kike anayejulikana kwa jina la Erika Do Rosario pindi alipokuwa mchezaji wa Leganes miaka ya 1997.

Kesi hiyo iliyofunguliwa tangu mwaka 2018 na Mama wa binti huyo rasmi sasa mahakama hiyo imetoa maamuzi kuwa binti Erika Do Rosario Nieves mwenye umri wa miaka 22 kuwa mtoto wa kumzaa wa gwiji huyo.

Katika utoaji wa maamuzi hayo ambayo Eto'o hakuwepo mahakamani hapo inadaiwa alikutana na Mama binti huyo kwenye klabu moja ya usiku mwaka 1997 wakati ambao alikuwa akiichezea klabu ya Leganes kwa mkopo akitokea Real Madrid.

Baada ya maamuzi hayo Eto'o ameamuriwa pia kulipa kiasi cha euro 1,400 kwa mwezi kwa ajili ya matumizi mbalimbali huku akitakiwa pia kufika mahakamani pindi atakapohitajika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live