Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majibu ya Abdi Banda baada ya kupima Corona

99445 Pic+banda Majibu ya Abdi Banda baada ya kupima Corona

Thu, 19 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Banda anayecheza Highlands Park ya Afrika Kusini amegundulika hana maambukizi virusi vya ugongwa wa Corona.

Banda alisema alifanyiwa vipimo vya afya baadaya kujihisi anaugonjwa huo, lakini majibu ya vipimo vimeonyesha kwamba hajaambukizwa corona.

Banda alisema anamshukuru Mungu kwa kumnusuru na virusi hivyo hatari ambavyo vinaisumbua dunia kwa sasa.

"Nilikuwa nikijihisi kuumwa nikachukua hatua za kujitambua kwa kufanyiwa vipimo, jambo jema ni kuwa majibu yametoka ni nipo salama."

Muda mchache baada ya mazungumzo hayo, Banda alienda katika ukurasa wake wa mitandao ya Kijamii na kuandika ujumbe uliosomeka, "Napenda kutoa shukrani zangu kwa wote mlioguswa au kustushwa na habari juu yangu."

"Kikubwa kila kitu kimeenda sawa na kwa baraka za Mungu imegundulika kuwa haukuwa ugonjwa unaosumbua duniani. Asanteni sana na Mungu awabariki."

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Hata hivyo Banda alisema ni vyema Watanzania wakaendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo hatari.

"Tahadhari inatakiwa kuwa kwa mmoja mmoja tukifanikiwa katika hilo tutaushinda ugonjwa huu. Tunatakiwa kuwa wasikivu kwa kufuata taratibu mbalimbali za kijihadhari kama vile ambavyo viongozi wetu wamekuwa wakituelekeza," alisema.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametangaza leo ongezeko la wagonjwa wawili wa virusi vya Corona, mmoja amekutwa Zanzibar na mwingine jijini Dar es Salaam wote ni raia wa kigeni.

Jumla sasa wamefika watatu huku akifunga shule na vyuo vyote nchini pamoja na kusimamisha kwa michezo mbalimbali.

Chanzo: mwananchi.co.tz