Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeraha yamuondoa nyota wa Argentina Kombe la Dunia

8924 MAJERAHAAA TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mchezaji wa Argentina, Manuel Lanzini atazikosa fainali za Kombe la Dunia msimu huu wa kiangazi nchini Russia baada ya kupata majeraha.

Nyota huyo wa West Ham mwanzoni mwa mwezi Machi, Lanzini aliifungia timu yake ya bao la kwanza ilipokuwa ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Italia ambako iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Shirikisho la Soka Argentina, imeeleza kwamba mchezaji huyo amemepata majeraha kwenye mazoezi ya kikosi hicho leo Ijumaa asubuhi, hivyo atazikosa fainali za Kombe la Dunia Russia.

Lanzini amefunga jumla ya mabao 29 msimu uliopita kwenye klabu yake ya West Ham.

Argentina inayonolewa na kocha Jorge Sampoli ipo kundi D na itatupa karata yake ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia katika mchezo utakaowakutanisha na Ice Land Juni 16.

Pia itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Crotia Juni 21 na itashuka dimbani tena kumenyana na Nigeria Juni 26.

Chanzo: mwananchi.co.tz