Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa kushiriki Kili Marathoni

Majaliwapic Majaliwa atashiriki mbio fupi za Km 5

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 20 ya mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2022.

Taarifa iliyotolewa na waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Marathon ilisema Waziri Mkuu ataongoza maelfu ya washiriki na watazamaji katika maadhimisho hayo ya miaka 20 Mjini Moshi Jumapili Februari 27, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Waziri Mkuu anatarajiwa kuongozana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na mkoa.

“Maandalizi yote yamefikia hatua nzuri huku tukisubiri kumpokea Waziri Mkuu katika maadhimisho haya ya miaka 20,” walisema waandaaji hao.

Kwa mujibu ya waandaaji hao, Majaliwa anatarajiwa kushiriki katika mbio za Grand Malt 5Km kabla ya kuendelea na shughuli za sherehe ya miaka 20 katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU).

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi, ambaye bia yake ni mdhamini mkuu wa Kilimanjaro marathon, alisema wanayo furaha kuungana na Waziri Mkuu katika maadhimisho ya miaka 20 kwani inaonesha uzito wa shughuli hii.

“Hii inaonesha ni jinsi gani Kilimanjaro Marathon imekuwa mwaka hadi mwaka na hata kuwavutia viongozi wa kitaifa,” alisema huku akitoa wito kwa washiriki kuendelea kujifua vizuri na kuhudhuria kwa wingi.

Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager (Mdhamini Mkuu) Tigo (21km) na Grand Malt (5km).

Wadhamini wa meza za maji ni pamoja na Absa Tanzania, Unilever Tanzania, TPC Sugar, Simba Cement na Kilimanjaro Water.

Wasambazaji rasmi ni GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel, CMC Automobiles na Surveyed Plots Company Ltd (SPC) na Bodi ya Utalii (TTB).

Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zinatarajiwa kufanyika Jumapili ya Februari 27, 2022, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), ambapo zimeandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Company Limited na kuratibiwa na wadau wa hapa nchini kampuni ya Executive Solutions Limited.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live