Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaamuru kukamatwa kwa Hans Poppe wa Simba

7244 Hans Poppe TZW

Tue, 1 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imetoa amri ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa usajili Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo.



Wawili ho wamedaiwa kutafutwa na Takukuru tangu mwezi March mwaka huu bila mafanikio yoyote.

Amri ya kukamatwa kwa Hans Poppe na mwenzake imetolewa leo na Hakimu Thomas Simba ambaye anasikiliza kesi hiyo baada ya Wakili Leonard Swai wa Takukuru kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.

Wakili Swai amedai amekuwa akiwatafuta washtakiwa hao toka mwezi March bila mafanikio. Washtakiwa hao wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu.

Loading...
Chanzo: bongo5.com