Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Yaamuru Lionel Messi Kubomoa Hoteli Aliyoiacha Barcelona

0fgjhs4ajb1uhf74i Mahakama Yaamuru Lionel Messi Kubomoa Hoteli Aliyoiacha Barcelona

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache tu baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora duniani (Ballon d’Or) kwa mara ya saba, Lionel Messi ameamrishwa na mahakama kubomoa hoteli yake ya kifahari iliyo katika jiji la Barcelona nchini Uhispania.

Kwa mujibu wa ripoti za majarida ya Mirror na Confidencial, hoteli ya Messi jijini Barcelona, agizo limetolewa na mahakama inayodai hoteli hiyo ilifeli kuafiki viwango hitajika. Messi aliondoka FC Barcelona mwanzoni mwa msimu na aliinunua hoteli hiyo yenye vyumba 77 vya kulala mwaka 2017.

Agizo hilo ni la kumvunja moyo Messi ambaye alipiga soka ya kulipwa nchini Uhispania kwa zaidi ya miaka 20 kabla ya kutua katika jiji kuu la Ufaransa, Paris.

Ripoti hiyo inasema kuwa hoteli hiyo tayari ilikuwa inapangiwa kubomolewa Messi alipoinunua kwa kitita kibubwa cha fedha mwaka 2017 japo hakujua.

Nyota huyo wa Paris Saint-Germain anatarajiwa kutuma mawakili wake kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya mahakama na kujaribu kutafuta mbinu mwafaka ya kumaliza utata huo bila ya kupoteza mali yake.

Messi amekuwa na wakati mgumu uwanjani tangu kuhamia Ufaransa na amefungia PSG goli moja pekee katika ligi kuu ya taifa hilo.

Awali, iliripotiwa jinsi nyota wa Manchester United na hasimu wa jadi wa Messi Cristiano Ronaldo alivyoelekea kwenye mitandao ya kijamii kudai kuwa Messi alikuwa amemwibia Robert Lewandowski tuzo ya mchezaji bora duniani mwaka 2021.

Messi alikabidhiwa tuzo ya Ballon d’Or usiku wa Jumatatu ya Novemba 29, lakini mashabiki wengi wa soka wakafokea shirika la France Football kwa kupuuza Robert Lewandowski.

Ronaldo ambaye ameshinda tuzo hiyo mara tano, alimaliza katika nafasi ya sita baada ya kupata kura 435.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live