Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maguli: Kwa Zesco, Yanga wawe makini mashambulizi ya pembeni

76534 Pic+maguli

Fri, 20 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

ELIAS Maguli kwa sasa anaitumikia Nakambala Leopard ya Zambia, amewapenyezea siri Yanga namna yakuwamudu wapinzani wao Zesco watakaocheza nao Septemba 28 mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pamoja na timu yao kuchapwa mabao 3-0 na Zesco, Maguli aliamua kuwa mzalendo wa kuwasoma wapinzani wao ili kuwapa siri Yanga namna ya kushinda mechi hiyo.

Amesema jamaa ni wazuri kwa mashambulizi ya pembeni, wanacheza pasi ndefu na fupi pia wanatumia kaunti ataki na kuwataka Yanga wapate muda wa kuwasoma nyota hatari kwao.

"Mabao tuliofungwa sisi yalikuwa ya mashambulizi ya pembeni katika mchezo na Yanga ninachokifikiria ni Zesco watakuwa wanacheza kaunti ataki ili kuwalazimisha Yanga kufanya makosa"

"Mawinga wao wana kasi na ndio waliotunga kwa namna hiyo, lazima Yanga watulie ili kupata ushindi dhidi ya hawa jamaa,lasivyo wanapaswa kujua kwamba sio wepesi"

"Soka la Zambia lina ushindani wa hali ya juu,yote katika yote naamini Yanga watasonga mbele kwani wao na Azam FC ndio waliobakia kuliwakilisha taifa letu kwenye michuano ya kimataifa"amesema.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz