Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli alihimiza viongozi wote wa michezo kuwajibika 

192c86cb70c7f9dd2f9dddd543aeaf38.png Magufuli alihimiza viongozi wote wa michezo kuwajibika 

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

OFISA Michezo Wilaya ya Ilemela, Kizito Bahati ’Sosho’ amesema Rais John Magufuli alihimiza uwajibikaji na uwazi kwa viongozi wa michezo katika ngazi tofauti.

‘’Alileta heshima kwa kila kitu katika nchi yetu akimaanisha wale waliokuwa katika sekta ya michezo kuwa makini na alikuwa akisikitika sana timu zetu za taifa zilipokuwa zikifanya vibaya,’’ alisema Kizito.

Alisema Rais Magufuli alitoa Sh bilioni 1 kwa ajili ya maandalizi ya Afcon kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.

Alisema Rais Magufuli pia alisaidia timu ya taifa katika kuwakumbusha uzalendo na kupambana kwa bidii wakati wote.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu, alisema pia Rais Magufuli aliwahi kutoa Sh milioni 50 kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu.

Alisema katika halmashauri na wilaya kulikuwa na ofisa utamaduni ambaye ndiye anayesimamia michezo yote, lakini katika utawala wake, Magufuli aliwaajiri maofisa michezo wa wilaya na kufanya eneo hilo kuwa na mtu sio kama zamani kulikuwa na ofisa utamaduni.

Alisema Magufuli pia alisaidia viwanja vya CCM Kirumba na Jamhuri Dodoma kuboreshwa.

Alisema kauli mbiu ya Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’, iliwajengea uwezo wachezaji wa michezo mbali mbali kuwa na ujasiri wa kupambana wakati wote wawapo katika mashindano mbalimbali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz