Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magori aaga Simba jumla

62586 Pic+magori

Thu, 13 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Crescentius Magori ametangaza kutoendelea kuitumikia klabu hiyo mara baada ya mkataba wake kumalizika.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini leo, Magori alisema aliteuliwa kushika nafasi hiyo kwa muda na kutokana na mapenzi yake na klabu hiyo alikubali wito huo ingawa hakuwa tayari kuhudumu.

"Nafasi ambayo nilipendezwa nayo zaidi ni kuwa mmoja wa wakurugenzi wa bodi na sio hii ya utendaji mkuu kwa sababu ninapokwenda kwenye vikao vya bodi mimi nakuwa msikilizaji tu ingawa nina hamu ya kutoa ushauri ambao utaisaidia klabu hiyo kupiga hatua.

Kwa hiyo sasa miezi sita imemalizika na mkataba wangu umemalizika, lakini kikao cha bodi kilichokaa jana wameniomba nihudumu kwa miezi miwili ya ziada ili kuweka sawa baadhi ya mambo mfano usajili na maandalizi na baada ya hapo nitangaze kuwa sitoendelea na nafasi hiyo.

Wakati nateuliwa nilikuwa mmoja wa wakurugenzi wa bodi hivyo kama ikiwapendeza wenyewe basi nitarejea kwenye nafasi hiyo lakini niwatoe wasiwasi Wanasimba kwamba Simba itapata Mtendaji Mkuu mpya bora pamoja na wakurugenzi ambao watamsaidia na nitashiriki kikamilifu katika kuhakikisha hilo linatimia.

“Ndani ya kipindi hicho cha miezi miwili ambayo nitahudumu baada ya mkataba wangu kumalizika, ndipo Mtendaji Mkuu Mpya atapatikana," alisema Magori.

Pia Soma

Magori alitamba kuwa anajivunia ndani ya kipindi hicho cha miezi sita, ametoa mchango mkubwa katika kuifanya Simba itambe kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kufanya usajili makini.

Chanzo: mwananchi.co.tz