Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magoli 10 makali ya 'usiku' Ligi Kuu

USIKU Magoli 10 makali ya 'usiku' Ligi Kuu

Mon, 13 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KUMEKUWA na ongezeko la magoli yanayofungwa dakika za nyongeza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa siku za hivi karibuni kuelekea kumalizika kwa msimu wa 2019/20.

Magoli hayo yamekuwa yakifungwa katika dakika ambazo tayari baadhi ya mashabiki wa soka wameshatoka nje ya uwanja, na wengine wameshapanda kwenye usafiri wao binafsi au ule umma.

Magoli haya yanatokana na sababu nyingi za waamuzi kuongeza dakika za nyongeza, ikiwamo wachezaji kuchelewesha muda na hasa makipa.

Ni magoli ambayo yameongeza utamu wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo tayari Simba imeshatwaa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo, huku baadhi ya timu zikishindana kukimbia kwenye nafasi nne za chini za kushuka daraja, na zingne mbili za juu yake ambazo timu zitakwenda kucheza mechi za mtoano.

Kutokana na kuwapo magoli yanayofungwa dakika za nyongeza kwa siku za karibuni, mwandishi wa makala haya amekukusanyia jumla ya magoli 10 yaliyofungwa kwenye dakika za majeruhi na wafungaji wake.

1. Peter Mapunda (Mbeya City vs Mbao) dk 90+3

Mbeya City ikiwa ugenini, iliichapa Mbao FC mabao 2-1, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini, Mwanza, mechi iliyochezwa Oktoba 28, mwaka jana. Wakati zilipofika dakika 90 timu hizo zilikuwa sare ya bao 1-1, lakini dakika tatu za nyongeza zilitoa matokeo tofauti kabisa. Mbeya City ilipata penalti na mchezaji Peter Mapunda akauweka wavuni na Mbeya City ikapata ushindi kwenye mechi hiyo.

2. Paul Bukaba (Namungo vs Coastal) dk 90+4

Hili lilikuwa ni bao la kujifunga. Ilikuwa ni dakika ya nne ya nyongeza, beki wa Namungo, Paul Bukaba alipojifunga mwenyewe na kuwapa wapinzani wao, Coastal Union ushindi wa mabao 3-1 Uwanja wa Majaliwa mjini Lindi, Novemba 22 mwaka jana.

Wakati wachezaji wa Namungo wakitafuta bao la kusawazisha dakika za majeruhi angalau iwe 2-2, Bukaba akajifunga mwenyewe na mechi ikaisha hivyo.

3. Haruna Chanongo (Mtibwa vs Kagera Sugar) dk 90+3

Novemba 26, mwaka jana, Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, ilizikutanisha timu ndugu, Kagera Sugar iliwapokea Mtibwa Sugar. Wakati Kagera Sugar ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, ikitafuta bao japo la kusawazisha mechi iishe kwa mabao 2-2, wakijikuta wakipachikwa bao la tatu, dakika ya tatu za nyongeza, likifungwa na Haruna Chanongo na mechi ikaisha kwa Mtibwa kushinda ugenini magoli 3-1.

4. Abdul Hillary (KMC vs Yanga) 90+3

Mashabiki wa Yanga walijua kabisa timu yao ingeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ngumu ya KMC.

Dakika tatu za majeruhi zilitoka kabisa kubadilisha matokeo na kuwa sare ya bao 1-1. Ni kwamba Kelvin Yondani alimdondosha mchezaji mmoja wa KMC ndani ya eneo la hatari na KMC ikazawadiwa penalti, ambayo iliwekwa wavuni na Abdul Hillary, ngoma ikaenda sare, mechi ikichezwa Desemba 2, mwaka jana.

5. Gerson Fraga (Simba vs KMC) dk 90+3

Mbrazil wa Simba Gerson Fraga naye yumo kwenye orodha ya wachezaji waliofunga magoli kwenye dakika za majeruhi. Yeye alifunga bao Desemba 28, mwaka jana, Simba ikiifunga KMC mabao 2-0.

Wakati Simba ikiwa inaongoza bao 1-0, huku baadhi ya mashabiki bado wakiwa hawaamini kama timu yao ingetoka uwanjani na ushindi huo, Fraga aliongeza bao la pili dakika ya tatu ya nyongeza na ubao ukasomeka 2-0.

6. Daudi Mbweni (Singida United vs Mbao) dk 90+4

Daudi Mbweni ni mchezaji wa Singida United ambayo kwa sasa imeshashuka daraja, inachofanya ni kumalizia mechi zao tu zilizobaki. Yeye aliweka rekodi ya kufunga bao kwenye dakika ya nne ya nyongeza, siku timu yake ilipobugizwa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Mbao. Hiyo ilikuwa ni Februari 18, mwaka huu.

7. Ayoub Lyanga (Coastal vs Lipuli) dk 90+4

Ni mechi iliyochezwa Machi 10, mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini, Tanga ikishuhudia mchezaji wa Coastal Union, Hance Rashid akifunga bao kwenye dakika ya nne ya nyongeza, Coastal ikiichapa Lipuli mabao 2-0. Wakati wachezaji wa Lipuli wakihangaika kutaka kusawazisha bao dakika hizo, Hance akaandika bao lililomaliza mchezo.

8. Patsons Shigala (Mbeya City vs JKT) dk 90+2

Mbeya City ilipata ushindi wa mabao 2-0 Juni 27 mwaka huu dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Bao la pili la washindi lilipatikana dakika ya pili ya nyongeza, likifungwa na Patson Shigala.

9. David Molinga (Yanga vs Namungo) dk 90+7

Straika wa Yanga, David Molinga aliiokoa Yanga isipoteze mechi dhidi ya Namungo Juni 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam. Wakati kila mmoja akijua Yanga imelala kwa mabao 2-1, Molinga alisawazisha bao kwenye dakika ya saba ya nyongeza na mechi hiyo ikaisha kwa mabao 2-2.

10. Cleophace Mkandala (Prisons vs Coastal) 90+8

Wakati ikidhaniwa kuwa bao la Molinga ndiyo litakuwa limeweka rekodi ya kufungwa kwenye dakika nyingi zaidi za nyongeza, ukweli siyo hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live