Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madeni ya Pluijm, Lwandamina, TRA yaitia umaskini Yanga

87913 Pic+madeni Madeni ya Pluijm, Lwandamina, TRA yaitia umaskini Yanga

Fri, 13 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dk Mshindo Msola amesema madeni fedha za usajili wa wachezaji, TRA pamoja na makocha George Lwandamina na Hans Pluijm yameifanya klabu hiyo iteteleke kiuchumi tangu walipoingia madarakani.

Madeni hayo ni fedha za usajili Sh254 milioni, TRA ni Sh800Milioni, wakati makocha Lwandamina anadai Dola 10,000, huku kocha Hans Pluijm akiwa anadai Dola 53,000 hadi sasa amelipwa Dola 8,000, mbali ya hayo kuna madeni binafsi Sh217 milioni.

Akizungumza makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Jangwani na Twiga Jijini Dar es Salaam, DK Msola alisema uongozi uliopita uliacha madeni mengi ya fedha za usajili pamoja na kuvunja mikataba ya makocha.

"Sisi wakati tunaingia tumekuta tunadaiwa, hii ni taasisi na unapoikuta ina kasoro unatakiwa uweke sawa, hivyo tulianza kulipa madeni hayo," alisema Msolla.

Msolla alisema kwamba madeni ya fedha ya usajili pamoja na malipo ya makocha yalikuwa makubwa na walitakiwa kuyalipa na ndio maana wamekuwa wakiteteleka.

"Tulikuta wachezaji hawajalipwa mishahara sisi kwetu tumejitahidi kulipa, tumekuta deni la fedha ya usajili Sh 254 milioni, pia tunadaiwa na TRA Sh 800Milioni," alisema Dk Msolla.

Aliongeza kwa kusema " fedha ya Serikali ilikuwa ni kwa ajili ya majengo na tulianza kuilipa, lakini mchezaji kama Youthe Rostand tumemlipa fedha yake yote Sh60Milioni hatudai."

Kiongozi huyo alidai kwamba licha ya Yanga kudaiwa na wachezaji pamoja na Taasisi zingine bado kuna watu binafsi wanaidai timu hiyo zaidi ya Sh 217Milioni ambalo ni deni wamelikuta wakati wanaingia katika klabu hiyo.

"Tunapitia magumu mno na mashabiki wanaweza wakawa hawayaoni haya, lakini tulikuwa na wakati mgumu katika hili kuhakikisha timu ikiwa bado inaendelea kuwepo," alisema.

Aliongeza kwamba kwa safari hii tangu wao waingie wamelipa wachezaji wote mishahara na wanadaiwa mishahara ya miezi miwili tu.

"Mpaka leo jioni mishahara itakuwa imeshaingia kwenye akaunti zao, tunakiri kweli hatukulipa, lakini wanalipwa fedha zao," alisema Dk Msolla.

Chanzo: mwananchi.co.tz