Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madega avunja ukimya Yanga

69808 Madega+pic

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

IMANI Madega, mmoja wa wenyeviti wa Yanga aliyeacha alama Jangwani hasa kwa kitendo cha kuondoka akiiacha akaunti ya klabu hiyo ikiwa imenona amevunja ukimya na kuwataka Wanayanga kushirikiana na viongozi wa sasa ili wazidi kupaa.

Madega alisema uongozi uliopo sasa chini ya Dk. Mshindo Msolla unaonekana kuwa na maono mapya, hasa katika uandaaji wa tamasha ya kila mwaka huwafanya wanayanga kukutana pamoja.

"Tamasha la 'Wiki ya Mwananchi' ni moja ya njia ya kuongeza mapato na kuacha dhana ya timu kuonekana ya watu wachache, ombi langu kwa uongozi kile kitakachopatikana kitumike vizuri, lakini wanayanga wauunge mkono uongozi kwa kila hali," alisema.

Madega alisema anapata matumaini timu hiyo kufanya vizuri msimu huu kutokana na namna uongozi ulivyoheshimu benchi la ufundi kwenye suala la kusajili wachezaji maana miaka ya nyuma viongozi walikuwa wakituhumiwa kuingilia majukumu hayo.

"Hatutakiwi kusema kitu gani kilituangusha nyuma, bali tunapaswa kutazama mambo ambayo yatatusaidi kupiga hatua zaidi ya hapa tulipofika sasa, kwani tunaamini Yanga imezaliwa upya."

Mkongwe huyo atakumbukwa zaidi kwenye misimamo yake tangu aingie madarakani Mei 30, 2007, kwani alikuwa mmoja wa viongozi waliopenda kuona soka la vijana linathaminiwa.

Yanga iliyoweka kambi mkoani Morogoro, leo Jumapili inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuhitimisha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya.

Baada ya mchezo huo, Yanga itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Township Rollers ya Botswana katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao walikutana nao mwaka jana na kulala 2-1 nyumbani kisha kwenda kutokla suluhu na kutolewa michuanoni.

Chanzo: mwananchi.co.tz