Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madagascar, Tunisia, Ghana zanusa Afcon2021

85165 Pic+afcon Madagascar, Tunisia, Ghana zanusa Afcon2021

Fri, 22 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Timu za Taifa za Madagascar, Ghana, Nigeria, Senegal, Algeria na Tunisia zimejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu ya kukata tiketi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2021 Cameroon kwa kushinda mechi mbili za kwanza za hatua ya makundi.

Timu hizo sasa zinahitaji pointi nne tu katika michezo minne iliyobakia ili kukata tiketi ya kushiriki Afcon.

Mkwaju wa penalti wa mshambuliaji Jordan Ayew, ulitosha kuipa Ghana ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Sao Tome & Principe uliochezwa juzi Jumatatu na kuifanya ifikishe pointi sita zilizoiweka kileleni mwa kundi C ambalo nafasi ya pili wapo Afrika Kusini na Sudan ipo nafasi ya tatu kila mojaikiwa na pointi tatu, huku timu ya Sao Tome & Principe wakihsika mkia wakiwa hawana pointi.

Mabingwa wa taji la Afcon mwaka huu, Algeria walijihakikishia uongozi wa kundi H baada ya kuibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Botswana juzi Jumatatu ambao umewafanya wafikishe pointi sita, nyuma yao wakiwepo Zimbabwe wenye nne, wakati Botswana na pointi yao moja wako nafasi ya tatu huku Zambia wakishika mkia hawana pointi.

Wanafainali wa Afcon mwaka huu, Senegal waliendelea kukaa kileleni mwa kundi I baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 ugenini dhidi ya Eswatini ambapo matatu kati ya hayo yalifungwa na Famara Diédhiou na lingine moja likipachikwa na Papa Ndiaye.

Katika kundi J, ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Guinea ya Ikweta uliendelea kuifanya timu ya taifa ya Tunisia ijikite kileleni wakifikisha pointi sita huku wakifuatiwa na Tanzania na Libya ambazo kila moja ina pointi tatu na Guinea ya Ikweta inashika mkia ikiwa haina pointi.

Nigeria nayo iliibukana ushindi wa mabao 4-2 ugenini dhidi ya Lesotho juzi Jumapili na kuifanya ifikishe pointi sita shukrani kwa mabao ya Alex Iwobi, Samuel Chukwueze na Victor Osimhen

Wakisaka nafasi ya kushiriki Afcon kwa mara ya pili, Madagascar waliipa kichapo kitakatifu timu ya Niger cha mabao 6-2 katika mchezo ambao ilikuwa ugenini.

Mabao ya Lalaïna Nomenjanahary, Anicet Abel, Chales Andriamatsinoro, Paulin Voavy na Jérôme Mombris yalitosha kuwafanya Madagascar wafikishe pointi sita na kuongoza kundi K lenye timu za Ethiopia, Ivory Coast na Nigeri.

Lakini hali ikiwa hivyo kwa timu hizo, Misri wanaoongoza kutwaa taji la Afcon wakifanya hivyo mara saba, wameendelea kusuasua baada ya kulazimishwa sare ya pili dhidi ya Comoro, katika mchezo ambao ulichewa ugeni huko Visiwani Comoro, juzi Jumatatu.

Chanzo: mwananchi.co.tz