Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maboresho tuzo Ligi Kuu kiboko

9860 Maboreesho+picha TZWeb

Sun, 24 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kamati ya tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara imesifu na kuyapa tano maboresho yaliyofanyika katika mchakato wa kupata washindi mbalimbali wa tuzo za ligi hiyo msimu 2017/2018.

Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hizo, Alhaji Msafiri Mgoyi alisema kamati imefanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa tuzo za msimu wa 2017/2018 zinakuwa na mabadiliko makubwa tofauti na awamu zilizopita.

" lengo la tuzo hizi ni kuongeza hamasa na ushindani kwenye ligi hivyo niseme kamati ilihakikisha inaendesha zoezi kwa umakini wa hali ya juu ili kupata washindi sahihi.

Vipo vigezo mbalimbali ambavyo tumeviweka katika kupata washindi lakini kubwa zaidi ni muda ambao muhusika amekuwepo kwenye ligi na mchango alioutoa," alisema Mgoyi.

Chanzo: mwananchi.co.tz