Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabondia 6 kutoka nchi tatu kuwania mikanda ya kimataifa Dar

4503 Screen Shot 2018 03 09 At 16.51.07.png TZW

Mon, 12 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Wapenzi na wadau wa mchezo wa masumbwi nchini hapo kesho wanatarajia kushuhudia mapambano matatu makubwa na yakihistoria yatakayofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam, bondia Watanzania Cosmas Cheka akiwania ubingwa wa International Champions,  dhidi ya Salimu Mtango uzito wa kilo 59.



Mapigano mengine ambayo yanajumuisha nchi tatu bondia kutoka Tanzania, Saleh Mtalekwa atapambana na mwanamasumbwi wa Uganda, Weiswe Juma kuwania ubingwa wa Afrika kilo 67 huku mwana dada Alima Vunjabei akipambana na Nicholine Achieng kutokea Kenya pigano la Mkanda.



Katibu wa PST, Anton Luta amesema kuwa michezo yote hiyo itapigwa kuanzia majira ya saa 11:30 jioni uwanja wa ndani wa Taifa huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.



 

 

 

Chanzo: bongo5.com