Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabingwa wa Kombe la Dunia la Raga wa Afrika Kusini wakaribishwa kishujaa

Mabingwa Wa Kombe La Dunia La Raga Wa Afrika Kusini Wakaribishwa Kishujaa Mabingwa wa Kombe la Dunia la Raga wa Afrika Kusini wakaribishwa kishujaa

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Timu ya raga ya Afrika Kusini imerejea nyumbani kutoka Ufaransa baada ya kushinda kombe la dunia.

Wachezaji hao walikutana kwenye Uwanja wa Ndege wa OR Tambo mjini Johannesburg na umati mkubwa wa watu wenye furaha siku ya Jumanne.

Afrika Kusini ndiyo timu iliyofanikiwa zaidi katika Kombe la Dunia baada ya kushinda mataji manne katika mechi nane.

Nahodha Siya Kolisi alisalimiana na wafuasi katika uwanja wa ndege na Kombe la Webb Ellis, lililoshinda Jumamosi baada ya mchuano mkali dhidi ya New Zealand.

Aliuambia mkutano na waandishi wa habari mnamo Jumanne huko Johannesburg: "Tulifanya uamuzi kwamba tayari tuna Kombe la Dunia moja mnamo 2019. "Tulitaka kuhakikisha kuwa hii ni ya watu wa Afrika Kusini. Hii ni ya kila mtu wa Afrika Kusini. Tajiri, maskini... haijalishi unatoka wapi.

Chanzo: Bbc