Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabilioni ya Fifa yatua TFF, wampotezea Wambura

39864 Pic+fifa Mabilioni ya Fifa yatua TFF, wampotezea Wambura

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), liko mbioni kupokea fungu la maendeleo kutoka Shirikisho la Kimataifa (Fifa) huku vigogo hao wakimpotezea aliyekuwa rais wa TFF, Michael Wambura ambaye alifungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu.

Akizungumzia kwenye Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Rais wa TFF, Wallace Karia alisema, tayari Fifa imeridhia kutoa fedha za miradi ya maendeleo.

“Bila kueleza ni kiasi gani, Karia alisema fedha hizo zitaelekezwa katika miradi mbalimbali ikiwamo ya ukarabati wa Uwanja wa Karume na kujenga kituo cha mafunzo, Tanga.

Nje ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau aliliambia gazeti hili kwamba wanatarajia kupata Dola 5 milioni ambazo ni sawa na Sh 11 Bilioni kutoka Fifa.

Hata hivyo, katika mkutano wake wa Kigali, Rwanda uliofanyika Oktoba 26, 2018, Fifa ilitangaza kuwa kila mwananchama atapata Dola 6milioni. “ Tunatarajia kupokea fedha hizo wakati wowote ambazo ni Dola 3 milioni za awali ambazo zilizuiliwa na Dola 2 milioni za sasa,” alisema Kidau.

FIFA ilizuia kutoka fedha za miradi ya maendeleo TFF kutokana na ripoti chafu.

Hata hivyo, Rais wa Fifa, Gianni Infantino akiwa Kigali, Rwanda kwenye Baraza Kuu la Fifa, alisema kuwa Fifa ilipitisha maazimio ya Septemba kwa mipango ya maendeleo kwa wanachama wake 211 kwa mwaka 2019 hadi 2022.

Katika kipindi hicho, kila mwanachama atapata Dola6milioni ikiwa ni nyongeza ya Dola 1milioni ambazo ni kwa ajili ya uendeshaji wakati Dola 500,000 ni kwa ajili ya mambo 10 ikiwemo kuandaa mashindano ya vijana kwa wanawake na wanaume, ujenzi wa timu za taifa wanawake na wanaume pamoja na kuendesha program za waamuzi pia kwa wanawake na wanaume. Pia katika mpangilio huo, Dola 2 milioni kwa miaka minne, Fifa inataka zikamilishe miradi mbalimbali ambayo imeingiwa mkataba na Fifa kwa maendeleo ya soka na pia kila Shirikisho litapata Dola 12milioni kwa ajili ya maendeleo ya soka kwa jumla.

Fifa imeagiza fedha hizo kukaguliwa na kuwasilisha ripoti ya mapato na matumizi katika kipindi chote.

WAMPOTEZEA WAMBURA

Licha ya suala la Wambura kutazamiwa kuibuka kwenye mkutano mkuu wa TFF, baadhi ya wajumbe wa mkutano huo walipigilia msumari kifungo chake huku Rais wa TFF, Wallace Karia akisisitiza kuwa hawana habari na watu wanaojifanya kuwa wanaharakati wa mpira.

“Wacha waendelee kufanya uwanaharakati wao kwenye mpira, sisi tuachane nao,” alisema Karia huku akitolea ufafanuzi kwa wanachama kuwa wao TFF walikwenda mahakamani baada ya kupata wito huo lakini walienda kueleza nini ambacho kinaendelea.

KARIA AONYA

Akisoma hotuba yake katika mkutano huo uliofunguliwa na mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Karia alisema katika uongozi wake hatomfumbia macho yoyote atakayeonekana kuwaunga mkono watu walioiba fedha za Soka.

“Katika uongozi wangu nahitaji utawala bora na uwazi, nitakuwa mkali kwa yeyote atakayeonekana kuwaunga mkono watu walioiba fedha,” alisema Karia bila kutaja jina la mtu yoyote.

ATAKA REKODI AFCON

Katika mkutano huo uliodhuliwa na wajumbe zaidi ya 130, Karia alisema mikakati ya TFF ni kuona Tanzania inaweka rekodi ya kufuzu kucheza Afcon ya wakubwa, lakini pia timu ya vijana inafanya vizuri kwenye Afcon ya U-17 ambayo Tanzania ni mwenyeji.

“Timu ya vijana itakwenda Uturuki kwa maandalizi zaidi, lakini pia kuna mashindano yanatarajiwa kufanyika Rwanda, timu yetu itakwenda kwa ajili ya maandalizi zaidi,” alisema Karia.

Bosi huyo wa mpira nchi ni alibainisha kwamba amsha amsha za uenyeji wa Afcon zitaanza mapema wiki ijayo ili kuwahamasisha Watanzania kuwa tayari kwa mashindano yanayotarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Taifa, Uhuru na Chamazi.

ATAKA HISTORIA AWAMU YA 5

“Nahitaji kwenye utawala wa JPM, timu yetu ya soka iweke historia ya kufuzu kucheza Afcon, baada ya kufanya hivyo kwenye Afcon ya 1980 wakati wa Nyerere (Baba wa Taifa),” alisema Karia.

MKUTANO ULIVYOKUWA

Mapema Jana mkutano huo ulianza saa 3:49 Asubuhi ambapo wajumbe kutoka vyama vya mikoa mbalimbali, klabu za Soka na viongozi mbalimbali akiwamo rais wa heshima wa TFF, Alhaji Muhidin Ndolanga, Mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga wajumbe wa mkutano huo ulikuwa na ajenda 14.

Wajumbe walioneka kuwa watulivu wakifurahia huku baadhi wakigoma akizungumzia kutoalikwa kwa aliyekuwa makamu wa rais wa TFF, Michael Wambura ambaye walidai ishu yake ni ngumu na wanaiachia TFF ishughulike nayo.



Chanzo: mwananchi.co.tz