Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabao ya Tambwe, Makambo yaiondoa Tukuyu Stars FA

33285 Pic+matokeo Tanzania Web Photo

Mon, 24 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabao matatu ya Amis Tambwe yametokana na juhudi binafsi kwani Mshambuliaji huyo hakuyatarajia baada ya kufunga mabao ambayo si ya pasi huku Harietter Makambo akifunga bao moja kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tukuyu Stars. Hata hivyo Mshambuliaji huyo alikosa mabao mawili ambayo alipewa Pasi na Haruna Moshi na Pius Buswita huku akifunga mabao matatu ambayo hayakuwa ya pasi. Bao la kwanza Tambwe alifunga baada ya  kipa New Afrika kupangua hatari ya Fei Toto ikamkuta Tambwe aliyefunga. Bao la pili  Tambwe alijificha nyuma ya mabeki wawili wa Tukuyu ambao hawakumuona na kumalizia mpira wa krosi iliyopigwa na Buswita Kaseke akapiga kichwa ukamkuta Tambwe. Bao la tatu la Tambwe, Ibrahim Ajibu ndiye alikuwa na mpira kwenye nafasi ya kufunga lakini akateleza na Tambwe kuuwahi na katikati ya mabeki wawili wakati kipa wa Tukuyu ametoka

Chanzo: mwananchi.co.tz