Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabadiliko kikosi cha simba, Aussems aanzisha maproo wawili tu kuivaa Biashara United

77749 Pic+simba

Sun, 29 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Patrick Aussems amefanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake kwa kuwaanzisha wachezaji wawili tu wakigeni Pascal Wawa na Meddie Kagere, huku nyota tisa wakitanzania wakianza katika kikosi cha Simba dhidi ya Biashara United kwenye Uwanja wa Karume, mjini Musoma.

Mbali ya kuwaanzisha Wawa na Kagere, pia Aussems kwa mara ya kwanza atamtumia beki wake Kennedy Juma katika safu yake ya ulinzi leo dhidi ya Biashara United.

Katika safu ya kiungo Aussems leo amewaanzisha Said Ndemla, Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin ikiwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji wote wa kitanzania kuanza katika safu ya kiungo.

Kinara wa ufungaji Ligi Kuu, Kagere akiwa amefunga mabao matano katika mechi tatu, leo ataanza kama mshambuliaji pekee akisaidiwa na Ibrahimu Ajib.

Ajib anacheza mechi yake ya pili Simba tangu alipojiunga na mabingwa hao akitokea Yanga, hiyo ikiwa ni baada ya kuonyesha kiwango cha juu dhidi ya Kagera Sugar Alhamisi iliyopita.

Katika wachezaji wa akiba leo Aussems amewaka nje nyota watano wakigeni akiwamo Wabrazili wawili, Msudani Sharaf, Mkenya Kahata na Mkongo Kanda.

Pia Soma

Advertisement
Simba inaingia katika mchezo huo ikiwa na lengo moja tu la kupata ushindi na kuendelea kujikita kileleni ili kutimiza ndoto yake ya kutetea ubingwa wake.

Wapinzani wa Simba, Biashara United wanaingia katika mchezo wakiwa chini ya kocha wa msaidizi baada ya kumtimua kocha wake Amri Said ‘Stam’ kutokana na kupata matokeo mabaya.

Biashara United ipo nafasi ya 18, ikiwa imecheza mechi nne ikipata sare moja na kupoteza yote, imefungwa jumla ya mabao matano na kufunga bao moja.

Kikosi cha Simba; Aish Manula, Haruna Shamte, Mohamed Hussen, Pascal Wawa, Kennedy Juma, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Meddie Kagere na Ibrahimu Ajib

Akiba: Beno Kakolanya, Yussuf Mlipili, Tairone Santos, Gerson Fraga, Francis Kahata, Deo Kanda na Sharaf Shiboub.

Chanzo: mwananchi.co.tz