Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandalizi Uchaguzi Mkuu Simba yanoga

15827 PIC+UCHAGUZI+SIMBA TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Klabu ya Simba inatarajiwa ufanya uchaguzi wake Novemba 3 mwaka huu, huku maandalizi ya uchaguzi huo yakiendelea ikiwa ni pamoja na dirisha la wagombea kuchukua fomu kuwa wazi.

Wakati maandalizi mbalimbali yakiendelea uongozi wa klabu ya Simba umesisitiza kuwa katiba itakayotumika katika uchaguzi mkuu huo ni ile ya mwaka 2018.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Lyamwike, amesema kuwa katiba itakayotumika ni ya 2018.

Kiongozi huyo alisema ameamua kuweka msisitizo kutokana na baadhi ya wanachama kuendelea kuhoji juu ya katiba hiyo ambayo baadhi wanadai inawabana kwa baadhi ya vipengele haswa katika ngazi za elimu.

Wanachama hao baadhi walianza kuilalamikia katiba wakitaka kiwango cha elimu kwa mgombea Urais kiwe katika ngazi ya elimu ya kidato cha nne badala ya shahada kutoka chuo kikuu.

Simba walifanya mabadiliko kadhaa ya katiba hiyo na kusajiliwa na Msajili Mkuu wa Vyama vya Michezo ambaye pia alisema itatumika kwa shughuli zote za klabu ukiachana na ile ya zamani.

Tayari mchakato wa kuanza kuchukua fomu klabuni hapo upo wazi ingawa mpaka leo Jumatano hakukuwa na mwanachama yoyote aliyejitokeza kuchukua fomu.

Chanzo: mwananchi.co.tz