Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu ya Arusha United haya hapa

51678 ARUSHA+PIC

Thu, 11 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uongozi wa Arusha United umesema kuwa hautambui timu inayoendelea kushiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini kwa kutumia jina lao.

Arusha United ilicheza na Pamba ya Mwanza kwenye uwanja wa Nyamagana, Mwanza na kufungwa bao 1-0.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Ofisa Habari Arusha United, Jamila Omar alisema kuwa wameshangazwa sana kusikia kuwa timu hiyo imecheza mechi, huku uongozi wao ulikwisha tangaza kujitoa kwenye ligi na kuvunja mikataba ya wachezaji.

Jamila alisema kuwa wachezaji wote wamekwisha lipwa stahiki zao na kinachoendelea sasa katika timu hiyo kinawashangaza na hawajui kimetokea wapi.

“Mikataba ya wachezaji imevunjwa na hata kocha, Hemed Morocco naye amelipwa stahiki zake. Hawa wachezaji na timu iayotumia jina letu imetoka wapi wakati sisi hatupo kwenye ligi,” alihoji Jamila.

Alisema kuwa kinachoendelea sasa ni kinyume na utaratibu kwani hata bodi ya wadhamini wa klabu imeshangazwa na taarifa hizi.

“ Kuna jambo linaloendelea katika suala hili ambalo linatufanya tuanze kuhoji nani ameruhusu kutumia jina letu bila ridhaa,” alisema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto alisema kuwa bado hawatambui kujitoa kwa Arusha United kutokana na taratibu kutokamilika.

Mguto alisema kuwa waliwambia uongozi wa Arusha United kuwasilisha muhtasari wa kikao kilichopitisha maamuzi ya kujitoa na kushindwa kufanya hivyo.

“Labda huo muhtasari uliletwa TFF na Bodi ya Ligi wakati mimi nimeondoka kwenda Mwanza, lakini mpaka sasa sijaambiwa lolote kama huo muhtasari umefika , hivyo sis tunambua uwepo wa Arusha United kwenye ligi,” alisema Mguto.

Hata hivyo, mmoja wa aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Gaudence Mwaikimba alikiri kuwa mwajiri wao (Arusha United) amevunja mkataba na wao na anashangaa kusikia timu inacheza.

“Mimi sijacheza mechi dhidi ya Pamba kwa sababu uongozi wa Arusha United umevunja mkataba na sasa natafuta timu nyingine ya kuchezea msimu ujao. Nipo nyumbani Tabata naendelea na shughuli zangu nyingine,” alisema Mwaikimba.

Alisema kuwa hajui wachezaji gani wanaochezea timu hiyo kwani mwajiri tayari amevunja mkataba na kuwalipa stahiki zake.



Chanzo: mwananchi.co.tz