Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MO aahidi Sh100 Milioni, bodaboda Kilimanjaro Stars ikitwaa ubingwa

87907 Pic+mo MO aahidi Sh100 Milioni, bodaboda Kilimanjaro Stars ikitwaa ubingwa

Fri, 13 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampala, Uganda.Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji 'MO' amewaahidi wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kitita cha Sh 100milioni na bodaboda ikiwa watatwaa ubingwa wa mashindano ya Kombe la Chalenji yanayoendelea nchini Uganda.

Dewji ametoa ahadi hiyo katika kambi ya Kilimanjaro Stars aliyoitembelea usiku wa jana kwa ajili ya kuwapa hamasa akiwa ametembelea nchini hapa.

"Naamini mtafanya vizuri katika michezo yenu iliyobakia na mimi nawaahidi kuwapa zawadi ya Shilingi 100 milioni na pikipiki kwa kila mchezaji," alisema Dewji.

Bilionea huyo mbali na ahadi hiyo, alipiga picha ya pamoja na timu nzima kisha akafanya mazungumzo mafupi ya siri na nahodha Aishi Manula na mara baada ya mazungumzo hayo aliaga na kuondoka.

Stars leo itashuka uwanjani katika mchezo wake wa pili wa mashindano hayo yanayoandaliwa na kusimamiwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ambapo itakabiliana na ndugu zao wa Zanzibar 'Zanzibar Heroes'.

Timu zote mbili zilianza vibaya katika mechi zao za kwanza ambapo Kilimanjaro Stars ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Kenya wakati Zanzibar ilitoka sare ya bao 1-1 na Sudan

Chanzo: mwananchi.co.tz