Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MO Dewji aitaka Yanga Kombe la FA

98455 Pic+mo MO Dewji aitaka Yanga Kombe la FA

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ bado hajakubali na matokeo ya kipigo ilichopata timu yake kutoka kwa Yanga akiomba wakutana tena katika Kombe la FA.

Simba imefungwa bao 1-0 na Yanga katika mchezo wa pili wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, shukrani kwa bao pekee la Bernard Morrison.

Baada ya kipigo hicho MO Dewji leo kupitia ukurasa wake wa Twitter aliweka picha inayoonyesha takwimu za mchezo wa Yanga na Simba na kuandika ‘Hongereni Sana wana Yanga. Mungu akitujali tutakutana kwenye FA.’

Hii ni wazi kwamba MO Dewji na mashabiki wengi wa Simba bado hawajakubali na kipigo walichopata kutoka kwa watani zao Yanga jana.

Yanga iliingia katika mchezo huo ikiwa haipewi nafasi kubwa ya kushinda kutokana na rekodi zake za hivi karibu katika Ligi Kuu, lakini ilifanikiwa kuwaduwaza Simba mbele ya shabiki wao mkubwa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Shujaa wa Yanga katika mchezo huo alikuwa mshambuliaji Morrison aliyefunga bao kwa mkuja wa faulo uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa Aishi Manula akiwa hajui la kufanya.

Pia Soma

Advertisement

Ushindi huo unaifanya Yanga kuwa narekodi nzuri dhidi ya Simba baada ya mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa Januari 4, 2020, kutoka nyuma 2-0 na kusawazisha 2-2 matokeo yaliwapa nguvu wanajangwani.

Mapema leo Afisa Habari wa Simba, Haji Manara mtu aliyetaniwa zaidi na Wanayanga kwa kutumia picha zake mbalimbali, lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram alipongeza Yanga kwa ushindi.

Manara aliandika “Wanasimba wenzangu niwape salaam zangu fupi za kuwaomba kwanza tukubali tumepoteza mchezo wa jana kwa kufungwa na timu iliyocheza vzuri kuliko siye, na tukubali hilo halibadiliki kwa sasa, najua tumeumia ila hiyo ndiyo footbali tuliyoichagua kuipenda.

“Kwa tamaduni zetu lazima tucharurwe kama ambavyo tungewacharura iwapo tungeshinda, but life goes on, Muhimu kujipanga kwa mchezo unaofuata keshokutwa, tusitoke ktk reli na sote tunajua ubingwa upo mikononi mwetu, tusithubutu kumtafuta mchawi wala kulaumiana.

Wametufunga kihalali kabisa na ni haki yao kutamba!! Alimaliza kuandika ujumbe wake Manara.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz